Masharti ya Matumizi na Sheria za Jamii — Kilimo Heroes
Kilimo Heroes ni huduma ya Shechinah Limited, Tanzania. Ilisasishwa: 24 Novemba 2026. Kwa kutumia app, unakubali masharti haya.
Sheria za Jamii (hadithi za shamba na maudhui mengine unayoweka)
- Weka picha na maelezo ya kweli kuhusu kilimo chako.
- Hakuna nafasi kwa matusi, unyanyasaji, chuki, maudhui ya ngono au vurugu, ulaghai, matangazo ya udanganyifu, au taarifa za uongo kuhusu mbegu, mbolea na viuatilifu.
- Usiweke namba za simu, anwani au taarifa binafsi za watu wengine bila ruhusa yao.
- Usiweke maudhui usiyo na haki nayo.
Kuripoti na kuzuia
Kila hadithi ina kitufe cha ⋯: Ripoti hadithi au Mzuie mwandishi. Ukiripoti, hutaiona tena hadithi hiyo; ukimzuia mwandishi, hutaona tena hadithi zake. Hadithi ikiripotiwa na wakulima watatu hufichwa mara moja. Timu yetu hukagua kila ripoti ndani ya saa 24, huondoa maudhui yanayovunja sheria na kumfungia aliyeyaweka.
Ushauri wa kilimo
Bwana Shamba (msaidizi wa AI), Daktari wa Mazao na bei za soko ni msaada wa taarifa tu. Hakiki na mtaalamu wa kilimo kabla ya kutumia viuatilifu au kufanya maamuzi makubwa.
Akaunti
Unawajibika kwa akaunti yako. Unaweza kuifuta wakati wowote: Mimi → Futa akaunti yangu. Tunaweza kusimamisha akaunti inayovunja masharti haya.
Mawasiliano
Kuripoti jambo la dharura: privacy@shamba.africa · WhatsApp +255 739 300 777. Faragha: Sera ya Faragha.
English summary
By using Kilimo Heroes you agree to these terms. Post only genuine farming content. There is no tolerance for abuse, harassment, hate, sexual or violent content, scams, misleading adverts, false claims about seeds, fertiliser or pesticides, or other people's personal details. Every story has a ⋯ menu to Report it or Block its author: reported stories disappear for the reporter, stories reported by three farmers are hidden immediately, and our team reviews every report within 24 hours, removes violating content and bans the user who posted it. AI advice (Bwana Shamba, crop scan) is informational only. You can delete your account at any time (Me → Delete my account). Contact: privacy@shamba.africa.